Burudani

P Funk ni mtu poa sana hana ukali hata kidogo – Bongo Los

By  | 

Kundi jipya la muziki ‘Bongo Los’ limeeleza namna walivyokutana na prodyuza P Funk na namna wanavyofanya nae kazi kwa sasa na kusema prodyuza huyo ni mtu poa sana hana ukali hata kidogo, na si kama vile watu wengi wanavyomchukulia.

Bongo Los na P Funk

Member wa kundi hilo ‘Drew’ amesema watu wengi watasema P Funk ni mkali kama hawamfahamu, na kwa sababu unakuwa wanashtushwa na muonekano wake.

“Ni bonge la mtu alafu amejaa, ana matatoo lazima uogope, lakini kwa kawaida ni mtu poa sana, hana ukali hata kidogo. Hajawahi kuzingua kwa sababu tukiwa kazini tunafuata ile mienendo ya kazi kama tupo ofisini,” Drew amekiambia kipindi cha Planet Bongo.

Bongo Los

Katika hatua nyingine, Tamu ameelezea jinsi walivyokutana na kuunda kundi la Bongo Los, na kusema P Funk ndiye aliyewakutanisha studio kwa juhudi zake binafsi.

Drew ameongeza kuwa haiwezi kuwa vigumu kwao kufanya kazi kwa sababu kila mtu ana uwezo, kwa hiyo wakiunganika mambo yanazidi kuwa juu.

“Isitoshe yeye demu na mimi men kwa hiyo tunapata mashabiki wa pande zote mbili, washikaji wanapenda demu zaidi, mademu wanapenda men zaidi.

“Mimi hapa nilienda kwa P Funk ilikuwa 2014, kwenye mitandao ya kijamii alipost anatafuta wasanii chipukizi wenye vipaji wamtumie kazi, mimi nikatimba na studio kabisa, akaniwekea na instrumental nikachana akaniambia nipo vizuri,” amesema na kuongeza.

“Tukaja kukutana tena 2016 akaniambia yupo tayari kufanya kazi na isitoshe mimi nilikuwa nafanya  zangu tu kazi kitaa nikasema siyo mbaya  kwa sababu anaona nina uwezo wa kufanya nae kazi na istoshe yeye legendary , ndio tukaanza,” amemaliza kwa kusema.

By Peter Akaro

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments