Burudani

P-Funk wa 2008 ni Mpya na si wa enzi zileee!

MajaniNi mengi yamekuwa yakisikika kuhusiana na mtu mzima P-funk a.k.a Majani kuhusiana na ukimya wake katika kazi, wapo waliosema Majani kachoka hawezi tena kurudia zama zake, wengine wanasema P-funk anaogopa upinzani ambao umejitokeza katika muziki wa Bongo fleva hasa kwa miaka ya hivi karibuni na mengi zaidi yasemwayo lakini ukweli kuhusiana na mchizi huyu leo unapatikana katika kurasa hizi za Bongo5.com.

MajaniNi mengi yamekuwa yakisikika kuhusiana na mtu mzima P-funk a.k.a Majani kuhusiana na ukimya wake katika kazi, wapo waliosema Majani kachoka hawezi tena kurudia zama zake, wengine wanasema P-funk anaogopa upinzani ambao umejitokeza katika muziki wa Bongo fleva hasa kwa miaka ya hivi karibuni na mengi zaidi yasemwayo lakini ukweli kuhusiana na mchizi huyu leo unapatikana katika kurasa hizi za Bongo5.com.

 

 

 

Akizungumza na mshika kalamu wa Bongo5.com P-Funk alielezea kwanza sababu za ukimya wake na kuda kuwa “nilikuwa nahitaji kupumzisha akili yangu kwani nimekuwa nikifanya kazi kwa muda mrefu sana bila kupumzika sasa kitaalamu hasa unapokuwa unapofanya kazi zinazihitaji ubunifu inatakiwa ifike kipindi upumzishe akili ili iweze kufanya kazi vizuri”

 

 

 

Aliongeza kwa kusema “kuwa hewani sana nako si kuzuri kwani watu wengi hupata fulsa ya kukuzoea na kukuchukulia poa ndio maana kamautachunguza ni wengi ambao wanajaribu kukopi kile nachokifanya na yote hii ni kwa sababu ya kuzoea kusikika bila ya mpangilio wowote” alisema P-funk huku akishushia soda yake aina Coke.

 

 

 
Aidha Majani aligusia sababu nyingine ya msingi ambayo imepelekea kuwa kimya ni majukumu ya kifamilia ambayo yote yanamlenga yeye kwani now-a-dayz mchizi ni baba wa familia yenye watoto watatu “kwanza nataka ijulikane kama naizimia sana familia yangu na muda mwingi nahitaji kuwa karibu nayo kwani ukweli ni kwamba unaokuwa hali flani ya ubunifu inapungua automatic kutokana na majukumu amabyo yanakuwa yanakukabili lakini sio ishu nimejipanga kikamilifu na narudi rasmi nikiwa na mfumo mpya kiutendaji ambao naamini utakuwa ni bora kuliko miaka mingine yoote niliyowahi kufanya kazi” – Majani.

 

 

 

Moja ya mikakati ambayo amejiwekea Supa Dupa Pordyuza huyu katika ujio wake huu ni kuwa hataki kufanya kazi na wasanii weeengi kwa wakati mmoja kama ilivyokuwa zamani isipokuwa atakachofanya ni kufanya kazi na msanii kwa awamu akishamtoa anashughulika na mwingine na hii inatokana na hali ya ushindani kibiashara pamoja na mabadiliko yaliyopo kwenye muziki wa kizazi kipya “ukweli ni kwamba muziki wa bongo umepoteza muelekeo hata kiwanda chake nacho hakieleweki it just like Bubblegum ikishaisha utamu baada ya muda mfupi inatupwa unachukua nyingine”

 

 

 

Licha ya kufanya kazi na wasanii wachache pia anatarajia kuchukua wasanii wanaochipukia lakini wawe wakali na kuwasaidia na lengo lake hasa ni kubali muonekano uliozoeleka katika muziki wa kizazi kipya ikiwa ni pamoja kuwasimamia kazi zao na kuhakikisha kila msanii ambaye atakuwa chini yake anapata haki yake ya kisanaa ambapo yeye mwenyewe atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha anafuatilia kwa mstari wa mbele kabisa.

 

 

 

“unajua this time nataka niwe natoka mwenyewe na kujimix street na kuangalia wale ambao naamini watanifaa na hapo baadae kidogo nitaanzisha talent show yangu ambayo nitakuwa nikichagua mwenyewe vijana wenye vipaji na kuwatoa kisanaa” alisema P-Funk.

 

 

 

Akizungumzia upinzani uliopo kwenye kiwanda cha muziki hapa nchini Majani amedai kuwa anafurahi sana kuona wingi wa wazalishaji wa muziki ambao wamejitokeza miaka ya hivi karibuni jambo ambalo lianamfanya aweze kufanya kazi zake kwa wasaa kwani hapo awali ilikuwa kila mtu alikuwa akikimbilia kwake na kupelekea anakuwa anafanya sana kazi bila kupata time ya kupumzika, lakini kwa sasa anaweza kufanya kazi kimpangili kutokana na jinsi ambavyo amejiandaa.

 

 

 

“unajua kila mtu ameingiza mguu katika Music, pia watu wanabebana sana bila kuangalia na kuzingatia viwango bora vya kazi na utendaji, kazi za wasanii zimekuwa nyingi kiasi kwamba zinachangia sana kufeli kwa muziki hapa nchini lakini kama tutakuwa tunafanya kazi chache na kwa kupeana nafasi naamini hali ya muziki wa Bongo fleva inaweza kukaa vizuri”-P-Funk.

 

 

 

Mpaka sasa prodyuza huyu ameshatafuta masoko nchi za nje ambapo ana mchongo wa uingereza ambao aliupata baada ya kuchaguliwa kama mfanya biashara bora wa muziki nchini Tanzania, aliweza kukutana na baadhi ya wadau ambao wako tayari kupokea bidhaa zake, halikadhalika nchini Nigeria, India, Malaysia n.k, “So huu wingi a kazi hapa nchini kwa kweli haunistui kabisa isipokuwa umenipa changamoto ya mimi kuweza kupanuka kiakili, kimawazo na kimtazamo ambapo naangalia kupeleka bidhaa zangu katika Next Lavel kwani ukitazama hakuna mdau ambaye yuko tayari kupoteza muda wake kupoteza time yake kufuatilia haki za wasanii, ndio maana nimejipanga sana hata show ambazo nitakuwa nikizifanya nataka ziwe zenye mpangilio na wasanii wapate haki zao” alisisitiza prodyuza huyu.

 

 

 

Majani anafahamu na kusikia maneno mengi ambayo yanasemwa kuhusiana na ukimya wake lakini kauli yake ni kwamba, siku zote hawezi kuishi kama watakavyo watu wengine isipokuwa anaishi kulingana na misingi ambayo ameshajiwekea pamoja na namna ya kuyakamilisha malengo yake “watu wanshindwa kuelewa kuwa muziki ni kama baiskeli kama unaweza unaweza tu haina mjadala hiyo na ndio maana naweza kuona wanavyokiaharibu kiwanda cha muziki hasa wale wanaonikopi kazi zangu na hii nayo inachangia sana ukimya wangu kwani waweza kusikia kazi iliyofanywa na ukahisi ni mimi kumbe sio na ndio maana niliamua kupumzisha akili ili niweze kurudi tofauti na nilivyozoeleka, lakini yote hii ni kwa kuwa nafanya vizuri ndio maana wanaiga but now am going to the next level”-Majani.

 

 

 

Aliwataja wasanii ambao amefanya nao kazi na wamefanya vizuri sana sokoni kuliko msanii yoyote nao ni Juma Nature na Ferouz “Dah hawa jamaa wamefanya na wanaendelea kufanya vizuri katika soko la muziki wa Tanzania, sasa nachotaka kukifanya kwa mwaka huu ndio nitakaoanza nao nadhani mpaka Mwezi wa tano albam zao zitakuwa tayari na hawa ndio watakuwa wa awamu ya kwanza katika ujio wangu”

 

 

 

Kingine anachofanya Majani ni kutengeneza albam yake taratibu lakini hana mpango wa kuiweka katika levo za kibongo kwani ana mpango wa kuifanya kama demo yake ambayo anatarajia kuifanyia kazi katika siku za baadae.

 

 

 

“Ninachotaka watanzania na wapenzi wa burudani kwa ujumla wakae mkao wa kuupokea ujio wangu kwani nitabadilisha mfumo uliopo na kuweka mfumo ulio sawa na wenye maslahi zaidi, kwani nitaweza kazi chache na zitakazofanya vizuri ile mbaya” Alimaliza Prodyuza P-Funk a.k.a Majani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents