Burudani

P The Mc aeleza lengo lake kwa Kajala

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, P The Mc amesema lengo la kumtaja muigizaji Kajala Masanja katika ngoma yake mpya ‘MademuWangu’ si kama vile baadhi ya watu wamekuwa wakitafsiri.

Akizungumza na E-Newz ya EATV amesema alikuwa akitafuta angle ili kupata mtiririko wa mistari yake lakini pengine nyuma ya hiyo angle kuna vingi ambavyo mtu mwingine anaweza kuviongelea.

“Kila mtu nimemuongelea kwa sifa zile ambazo watu wanamfahamu, pengine wakawa hawamfamu hivyo lakini vyombo vya habari kila siku utasikia yupo na dogo fulani, yupo na mchizi fulani,” amesema P The Mc.

Katika hatua nyingine alipoulizwa juu ya kauli yake ‘utasikia yupo na dogo/mchizi fulani’, hakutaka kuweka wazi jina la dogo/mchizi huyo zaidi ya kusema kuna wengine hawajui.

“Wengine mpaka majina siwajui lakini tukianza kufuatilia kwa undani tunaweza tukapa vitu vingi sana ambavyo hata yeye anavifahamu pia ,” amesema.

Nikaona bora moyo niweke kwa Kajala, siku nzima haonekani kumuona mida ya kulala/
Kutwa kwa mashosti, Sinza, Mwenge na Mbagala, na anachonikera ni kupigwa pigwa na mafala/

Hiyo ni msitari ambayo inapatikana katika ngoma hiyo ambayo imewataja wasanii na waigizaji maarufu Bongo kama Shilole, Wema Sepetu, Shamsa Ford,Snura, Jokate, Aunt Ezekiel na wengineo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents