Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

P The Mc amvaa Madee kukopi idea ya ngoma yao, aibua jipya ‘Kiba_100’ ya Rostam (audio+video)

Rapper wa kundi la SSK, P The Mc amefunguka kuhusu ngoma ‘Nanii’ ya msanii mpya wa Tip Top Conection, Gaza aliyoshirikiana na Madee ambayo idea yake inafanana na ngoma ‘Kama Nanii’ ambayo amefanya P The Mc, ZaiiD na Cjamoker.

P The Mc amesema idea ya ngoma hiyo inafanana kabisa na yao na si ngoma ya kwanza kwa mwaka huu kutokea kitu kama hicho.

Amesema katika mix tap yake na ZaiiD ‘Mwenge Kiwalani’ Roma na Stamina (Rostam) wamechukua idea ya ngoma zao mbili ambazo ni Miyeyusho na Gombania Goli.

“Tulifanya wimbo unaitwa Miyeyusho wao wakafanya Hivi AmaVile idea ilikuwa ni kubishana na mwisho wa siku vitu ambavyo tuliviongea nao wakawa wamevirudia. Tuliweka wazi tukasema sisi tunachohitaji si kutulipa ila ni ile recognition, hata kama idea kugongana watu wajue ni nani alianza, mwisho wa siku walikubali” amesema.

“Ikaja tukafanya ‘Gombania Goli’ ambao mimi na ZaiiD tulikuwa kila mmoja anamponda mwenzie ili amchukue demu, juzi tu Rostam wimbo wao mpya (Kiba_100) wameimba wanamgombania demu ambao umefanana kila kitu, ubishani ni ule ule lakini tulikaushia” amesisitiza.

P The Mc amesema ngoma hiyo ya pili hawakutaka kuizungumzia sana ili kutoonekana wanalalamika ila ilipotoka ngoma hiyo ya Madee imebidi kuvunja ukimya kwanii hilo ni tukio la tatu kwa mwaka huu.

“Mwisho wa siku tukiongea watu wanasema tatizo nyie miziki yenu haikwenda, haikufika mbali ila hawa wameweza kuifikisha mbali lakini bado haina maana kwa sababu sanaa ni ubunifu hata ukija kusambaa baada ya miaka 10 bado ni changu na nimefanya wa kwanza kwa hiyo usinipangie kifike wapi na wapi” P The Mc ameiambia Bongo5.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW