Shinda na SIM Account

P The Mc autamani utunzi wa Seduce Me katika hip hop

Rapper wa SSK, P The Mc amesema utunzi wa ngoma ya Alikiba ‘Seduce Me’ (maneno machache) ndio watu wanauelewa kwa haraka kitu ambacho wana-hip hop wamekuwa wakishauriwa.

Akizungumza na Bongo5 amesema Seduce Me ni wimbo wenye maneno machache sana, kwa hiyo mtu anakariri kwa haraka na maneno yake yapo wazi kwamba ukiusikia mara moja tu unaweza ukawa umeshauelewa na kuupenda hapo hapo.

“Siku hizi watu wanapenda vitu vyepesi hivyo ndio tunaambiwa kila siku na mashabiki kwamba una complicates sana ebu chana kitu ambacho tunaweza kukielewa kwa haraka na kukuelewa”  amesema.

P The Mc kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Mademu Wangu’ pamoja na ile ya kundi la SSK ‘Slow Down’.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW