Burudani

P The Mc: Nilichokifanya katika ‘Mademu Wangu’ sijawasingizia

Msanii wa Hip Hop Bongo, P The Mc anayewakilisha kundi la ‘SSK'(Sisi Sio Kundi) amedai kuwa alichokiimba katika ngoma ya ‘Mademu Wangu’ ya marehemu Ngwear ni kitu cha kweli.

Akiongea na Bongo5, P amesema alichokiimba katika ngoma hiyo ambayo ametaja majina ya mstaa ndicho kilichopo kwani wanafahamika kwa namna hivyo.

“Kutumia majina ya hao wasichana wa mjini ambao ni maarufu watu wengi wanafahamu, kwanza ilikuwa ni kurahisisha watu kuupokea wimbo kwa haraka kwa sababu wakiwasikia hao wanakuwa wameshajua na watu wanakuwa wameupokea kwa haraka.”

Akaongeza kuwa “Kwa kuwasikia hao wanakuwa wanajua demu fulani anatabia fulani, kwa hiyo mimi nilichofanya hao wasichana sijawasingizia wala sijawadhalilisha isipokuwa nimeongea ukweli wa maisha yao ambayo kila mtu anayafahamu kwa namna hiyo so kama watakuwa wameamaua kuni maindi watakuwa wameamua kwa sababu mimi ni P The Mc.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents