Michezo

Pacquiao ataka Mayweather aadhibiwe na liwepo pambano la marudiano kwa kukiuka masharti

Bondia wa Ufilipino, Manny Pacquiao ametaka kuwepo kwa adhabu na pambano la marudiano baada ya hasimu wake Floyd Mayweather kudaiwa kukiuka sheria za matumizi ya dawa wakati wa maandalizi ya mechi yao ya May mwaka huu.

150503005027-15-pacquiao-mayweather-0502-super-169

Bondia huyo aliyeshidwa kwa pointi na Mayweather jijini Las Vegas, amewataka maafisa wa michezo wa jimbo la Nevada kuadhibu bondia huyo wa Marekani.

Mayweather alidaiwa na United States Anti-Doping Agency (USADA) kuwa aliwekewa drip ya vitamin na madini kabla ya pambano hilo.

Kutokana na taarifa hiyo Pacquiao amesema anataka mpambano wa marudiano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents