Michezo

Pacquiao: Najua nitamdunda Mayweather

Bondia wa Ufilipino, Manny Pacquiao amewaambia mashabiki wake kuwa ana uhakika atamdunda Floyd Mayweather kwenye pambano lao linalongojewa kwa hamu la May 2.

281D6EB900000578-0-image-m-10_1430249480147
Manny Pacquiao akiwasalimia mashabiki wake jana

“Najua nitashinda pambano hilo kwenye ulingo,” Pacquiao aliuambia umati wa mashabiki wake “Hivyo kuweni watulivu.”

281DBE7B00000578-3059680-image-a-38_1430253105433

Pacquiao aliwasili jana jijini Las Vegas akitokea Los Angeles na kupokelewa na watu takriban 1000 walikusanyika kwenye hoteli ya Mandalay Bay.

Umati huo uliokuwa na wafilipino zaidi uliangalia video ya muziki ya bondia huyo na waliburudishwa kwa burudani mbalimbali kabla hajawasalimia.

281DF71500000578-3059680-image-a-46_1430255813943

Kwenye pambano hilo, Pacquiao atalipwa zaidi ya dola milioni 100.

Naye Mayweather anatarajia kulipwa takriban dola milioni 180.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents