Fahamu

Padri asimulia alivyolazimishwa kutengeneza mabomu na magaidi

Padri asimulia alivyolazimishwa kutengeneza mabomu na magaidi

Kwa miezi mitano mwaka 2017, kundi la kigaidi la Islamic State(IS) liliteka nyara mji wa Marawi uliopo kusini mwa Ufilipino. Miongozi mwa mateka wao, alikuepo padre wa kanisa katoliki, baba Chito ambaye alilazimishwa kutengeneza mabomu chini ya vitisho vikali. Matukio aliyopitia padre huyo yalimshtua sana, lakini bado ana matumaini kuwa wakristo na waislamu wanaweza kuishi pamoja kwa amani.

Ulikuwa muda wa chakula cha jioni katika msikiti wa Bato, na watu 20 walikuwa wamezunguka meza moja ndefu tayari kwa mlo. Upande mwingine walikuwa wamekaa magaidi 15 na upande mwingine alikaa padre Chito na wakristo wengine.

Ghafla mlio wa bunduki uliwashtua na kuanza kupambana.

Dakika chache baadae , risasi ilipigwa kwa mbali na wakarejea kwenye meza.

Utaratibu huo ulikuwa wa kawaida kwa muda wote wa kuwa mateka. Padre Chito aliweza kuelezea kuwa walikuwa wanaishi kama jumuiya ndogo ambao wanakula pamoja na kufanya kazi pamoja.

Aliwahi kuwasikia magaidi wakisema kuwa lazima mmoja wao afe akipigana na jeshi la Ufilipino, jambo ambalo lilimuhuzunisha sana.

Grand mosque in Marawi, under fire in June 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Padre Chito alichukuliwa mateka tarehe 23 Mei 2017, siku ambayo mji wa Marawi ulipovamiwa na kundi la kiislamu la IS.

Kabla Marawi ulikuwa mji unaopendeza kwa majengo marefu ya kifahari na misikiti yenye kuvutia.

Ni mji ambao ulikuwa na waislamu wengi katika nchi yenye wakatoliki wengi.

Uislamu ulianza kusini mwa Ufilipino karne ya 13 kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nchi za uarabuni.

Ukatoliki uliingia nchini humo karne ya 16 baada ya ukoloni kutoka Hispania kuwasili Ufilipino na kushindwa kutawala eneo la kusini mwa nchi hiyo.

Tangu wakati huo waislamu wengi walioishi kusini walihisi kutengwa. Lilikuwa eneo ambalo wanaishi watu masikini zaidi katika taifa hilo na nguvu nyingi za kanisa katoliki zilionekana kuupendelea mji wa Manila.



Wakati ambapo padre Chito alipotuma kuhudumia eneo hilo la kusini miaka 23 iliyopita kwa lengo la kuboresha uhusiano baina ya wakristo na waislamu, mjadala mkali ulitokea.

Na mwaka 2017, mashambulizi ya kigaini yaliongezeka zaidi siku hadi siku mpaka mji wa Marawi ulipowekwa mateka kabisa.

100,000 people remain in campsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMiaka miwili baadae watu 100,000 walipotea baada ya uvamizi wa eneo hilo

Padre Chito alipata msukumo mkubwa kutoka kwa marafiki zake waislamu kwa wakristo kuwa lazima aondoke Marawi mapema iwezekanavyo, lakini badala yake aliamua kusali.

“Nilijiambia mwenyewe kuwa anamuachia kila kitu kwa Mungu hivyo sitakimbia”Padre Chito alieleza

Bato mosque (October 2017)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMsikiti wa Bato, sehemu ambayo padre aliwekwa mateka

Lakini kulikuwa na maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama katika mji huo, ambao hawakutaka kuwaunga mkono IS.

Siku za kwanza za utekaji, hali ilikuwa mbaya sana. Watu walikuwa na hofu sana na walikuwa wanatafuta njia ya kutoroka na huku wengine walibaki kujifungia ndani kwa kuogopa vurugu.

Padre Chito ilimbidi kutoka nje ili kusaidia watu licha ya kujua kuwa alikuwa anaweka maisha yake hatarini lakini alijiona kuwa hana njia nyingine zaidi ya kujaribu kusaidia.

Airstrikes in June 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Padre Chito alikamatwa na kuwekwa mateka na watu wengine 100 katika msikiti uliojulikana kama Bato.

Waliambiwa kama hawataonyesha ushirikiano watafundishwa adabu.

Padre Chito alielewa kuwa wanamaanisha kuwa watamtesa na hata kupoteza fahamu.Hivyo aliamua kufanya kazi ya kupika, usafi na kusaidia katika utengenezaji wa mabomu. F

Kuna wakati nilihisi nimeshindwa kusali bali nilikuwa ninamlalamikia Mungu kwa mateso ninayopitia pamoja na wenzangu.

Father Chito at the cathedral
The city in October 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionOktoba 2017

Kwa sasa padre Chito haishi tena Marawi mara baada ya kuokolewa mateka , anasema kuwa ni sehemu hatari sana.

Ingawa kuna wakati anatembelea ene hilo na kuongoza misa katika chuo kikuu au uenda katika eneo linalofahamika kwa wakristo ujumuika kwa wngi lifamikalo kama gymnasium na huko huwa anajihsi kuwa na amani.

Father at Chito at church in university gymnasium

Kwa mujibu wa BBC. Padre Chito amejipatia umaarufu mkubwa kwa huduama yake na wanafunzi huwa wanapanga foleni kupiga naye picha.

Padre anasema kuwa ana furaha sana kwa kupona katika utekaji ule na anaamini kuwa kadri muda unavyoenda ndio anapona jeraha alilopata .

Baada ya vita, watu wamejifunza mengi, Kwa sababu vurugu haiwezi kumpa ushindi mkristo wala muislamu bali wote watashindwa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents