Michezo

Mwamuzi wa pambano la Simba na Yanga ni mwanamke

Gumzo kwa sasa hapa Tanzania kwa wapenzi wa Soka ni kuhusiana na Mechi kubwa ya watani wa Jadi katika ya Yanga na Simba itakayofanyika mwishoni mwa juma lakini lingine kubwa zaidi sasa linalojadiliwa ni baada ya shirikisho la Soka nchini humo kutangaza kuwa mwamuzi wa mchezo huo ni mwanamama Jonesia Rukiyaa kutoka Kagera atakayekuwa pia akisaidiwa na atasaidiwa na Josephat Burali wa Tanga na Samuel Mpenzu wa Arusha.

okwi na refa

Refa wa akiba atakuwa Elly Sasii wa Dar es Salaam, wakati Kamisaa atakuwa mshambuliaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza, Khalid Bitebo ‘Zembwela’..

Mitandao inasema mwanadada huyo ni mmoja wa marefa ambao wanasimamia sheria za uwanjani kwa hakika bila kupindisha na kwa kawaida mchezo kati ya Yanga na Simba huwa ni mchezo wenye joto la hali ya juu.

Na viingilio vya mchezo wa huo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba SC na Yanga SC utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, huku kiingilio cha chini kikiwa ni Shilingi elfu saba tu (7,000).

Kiingilio cha juu cha mchezo huo kitakua shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents