Habari

Panda 2019 Initiative yafikia hatua nyingine ya usimamizi na muongozo wa ushauri na mawazo katika biashara

Wasichana 25 wamepata washauri na wasimamizi ambao watakuwa wanawaongoza na kuwasaidia kimawazo katika kuendesha biashara zao wanazotegemea kuzianza baada ya kumaliza mafunzo.

Wasichana hawa wametoka kumaliza mafunzo ya vitendo katika vipengele vya Mapambo,Mapishi,kilimo cha mbogamboga, na kucha, kupitia mradi wa Panda wa mwaka 2019, wenye lengo la kuwawezesha wasichana kwa kuwapatia ujuzi na muongozo ili waweze kujiajiri na kujitegemea kiuchumi, mradi huu unaoendeshwa na Shirika la Her Initiative.

Wasichana hawa walio kwenye mafunzo wameingia kwenye hatua hii nyingine ya Usimamizi na Muongozo wa mawazo na ushauri katika biashara . Usimamizi huu utafanyika kwa muda wa miezi mitatu.

Washauri na wasimamizi ni vijana ambao wanafanya biashara lakini pia ni vijana ambao wanaelewa changamoto zilizopo katika soko la biashara na wateja wanataka nini. Wasimamizi hawa ni Antu mandoza., Rahma Bajuni pamoja na Redemptus Caesar.

“Tunaamini wasichana hawa watapata muongozo na ushauri sahihi wa kimawazo kutoka kwa wasimamizi wao ambao wanauzoefu na wamepitia changamoto mbalimbali katika soko la biashara ”Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shirika la her initiative aliongea haya.

HER INITIATIVE ni shirika lisilo la kiserikali na si la kibiashara.Shirika hili limeanzishwa kwa lengo la kuwaelimisha wasichana katika jamii ili waweze kujitambua na kushiriki katika harakati zote za kijamii zinazohusu au kugusa maisha yao.

Dhamira kuu ya shirika hili ni kuwaelimisha na kuwapa wasichana kipaumbele katika jamii ili kuchochea maendeleo ya usawa na kuweza kujitegemea kiuchumi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents