Panya waharibu ofisi ya Rais

Baada ya kurejea siku ya Jumamosi akitokea nchini Uingereza, alipokuwa akipatiwa matibabu kwa muda wa miezi mitatu Rais wa Nigeria Muhammed Buhari anatarajiwa kuhamisha ofisi yake kwa kuwa imeshambuliwa na panya.

Kufuatia hali hiyo Buhari atalazimika kufanyia kazi nyumbani kwake kwa muda wa wiki tatu, mpaka hapo matengenezo ya kiyoyozi pamoja na fanicha kukamilika.

Msemaji wa rais amesema kuwa kitendo cha rais huyo kuhamisha kazi zake nyumbani hakita athiri utendakazi wa kiongozi huyo kwa njia yoyote.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW