Burudani ya Michezo Live

Papa Benedict agusia swala makasisi kufunga ndoa

Kiongozi mstaafu wa Kanisa Katoliki Papa Benedict wa 16 ametetea suala la makasisi kutofunga ndoa wakati ambapo mrithi wake anafikiria kulegeza marufuku hiyo kwa wanaume wanaooa ambao wanahudumu kama makasisi.

Pope Francis and Pope Benedict embracing in the Vatican

Papa Benedict amesema hayo katika kitabu walichoshirikiana na Kadinali Robert Sarah.

Hatua hiyo inawadia kujibu pendekezo la kuruhusu wanaume waliooa kutawazwa kama makasisi katika eneo la Amazon.

Papa Benedict, ambaye alistaafu mwaka 2013, amesema hakuweza kunyamazia suala hilo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Katika kitabu hicho, Papa Benedict amesema kutofunga ndoa kwa makasisi ni utamaduni wa kale ambao umekuwepo kwa karne nyingi tu ndani ya kanisa hilo, una umuhimu mkubwa kwasababu unaruhusu makasisi kuangazia majukumu yao.

Papa Benedict mwenye umri wa miaka 92 amesema “Halionekani kuwa jambo linalowezekana kutimiza majukumu ya ukasisi na ndoa kwa wakati mmoja”.

Ni nadra sana kwa Papa Benedict ambaye alikuwa wa askofu wa kwanza kujiuzulu katika kipindi cha karibia miaka 600, kuingilia masuala ya ukasisi.

Vatican bado haijasema lolote kuhusu na kitabu hicho, ambacho kiliangaziwa kidogo katika gazeti la Ufaransa la Le Figaro kabla ya kuchapishwa leo Jumatatu.

Wachambuzi wa Vatican wameshangazwa na hatua ya Papa Benedict kuingilia suala hilo, na kuongeza kwamba hatua ya Papa Benedict inavunja utamaduni ambao umekuwepo.

“Papa Benedict siyo kwamba anavunja ukimya wake kwasababu hakuhisi kwamba anavunja ahadi kwa kiapo alichokula. isipokuwa amekiuka kabisa,”Massimo Faggioli, mwanahistoria na mwanatheolojia. katika chuo kikuu cha Villanova ameandika katika mtandao wa Twitter.

Maoni ya papa Benedikto yalielezewa kama ya kushangaza na Joshua McElwee, mwanahabari wa gazeti la National Catholic Reporter.

Mwanathiolojia mwenye msimamo mkali ambaye anashikilia mtazamo wa tangu jadi na maadili ya kanisa amesema, Papa Benedict aliahidi kusalia kimya wakati anastaafu, akitaja hali mbaya ya afya.

Lakini tangu wakati huo, amekuwa akitoa maoni yake kupitia Makala, vitabu na mahojiano, akitaka papa Francis kuchukua njia tofauti, ambaye anaonekana kupendelea mabadiliko. Papa Benedict bado anaishi Vatican katika yaliyokuwa makao ya watawa.

Nini kilichopendekezwa kubadilika katika useja wa kidini?

Oktoba, Maaskofu wa Kikatoliki kutoka kila pembe ya dunia walifanya mkutano kujadiliana hatma ya kanisa hilo katika eneo la Amazon.

Katika kilele cha mkutano huo, kulitolewa ripoti yenye kuangazia masuala yanayoathiri Kanisa hilo na ndani yake, kukawa na pendekezo la kuruhusu wanaume walioa katika maeneo ya vijijini ya Amazon, watawazwe kuwa makasisi.Papa Benedict wa 16Papa Benedict wa 16 alistaafu Februari 2013 kwasababu ya matatizo ya kiafya

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW