Habari

Papa Francis aridhia ombi la Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania Kardinali Pengo la kustaafu, huyu ndio mrithi wake

Papa Francis aridhia ombi la Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania Kardinali Pengo la kustaafu, huyu ndio mrithi wake

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo ameng’atuka wadhifa huo na nafasi yake imechukuliwa na Askofu Mkuu mwandamizi, Yuda Ruwa’ichi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Charles Kilima, Askofu Pengo ameng’atuka baada ya kuomba kustaafu majukumu ya kuliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam ombi lililoridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko na kumteua Askofu Ruwa’ichi kushika nafasi hiyo.

Katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Miaka 75 ya kuzaliwa kwake, Askofu Pengo aliwaambia waumini wa Jimbo kuu la Dar es Salaam kwamba, anasubiria wakati wowote kumtii Baba Mtakatifu Francisko atakapomwambia kupumzika katika utume wa Kiaskofu. Askofu Pengo ameliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa miaka 27 tangu mwaka 1992 akimpokea Askofu Laurean Rugambwa.

Chanzo Mtanzania digital

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents