Habari

Papa Francis: Corona imefichua unafiki kati ya tajiri na maskini

Papa Francis anasema janga la virusi vya corona limeonyesha ni kwa jinsi gani maskini wametengwa na jamii.

Mara nyingi umaskini umekua ukifichwa, anasema, lakini kujaribu kuwasaidia wengine kunaweza kutusaidia kujitambua wenyewe.

”Mzozo huu wa virusi vya corona unatuathiri sisi sote, tajiri na maskini, na kuonyesha wazi unafiki, Nina wasiwasi unafiki a baadhi ya wanasiasa wanaoongea kuhusu jinsi wanavyokabiliana na mzozoz huu, kuhusu njaa duniani, lakini wakati huohuo wanatengeneza silaha”.amesema Papa katika mahojiano maalum na BBC.

Ameongeza kuwa huu ni wakati wa kuondokana na aina hii ya unafiki katika utendaji. Vinginevyo tuachane na imani zetu au tutapoteza kila kitu.

Papa Francis anasema kila mzozo una hatari na fursa kwa pamoja. Leo ninaimani kuwa tunapaswa kupunguza kiwango cha uzalishaji na ulaji na kujifunza kuelewa na kuitazama kwa makini duniahalisi. Tunahitaji kuwasiliana tena na mazingira yetu huu ndio wakati wa kuwa na mabadiliko.

”Ninaona uchumi ambao ni wa kiutu zaidi. Lakini tusipoteza kumbukumbu zetu tena pale janga hili litakapoisha,tusifunike yote yaliyotokea na kurejea tena tulikotoka ”,amessema Papa na kuongeza kuwa huu ni wakati wa kuchukua hatua za kimaamuzi, za kuachana na matumizi au kutumia vibaya mazingira wakati yote haya yatakapoisha. Amewataka wakazi wa dunia kutafakari na kushukuru kwa mali asili za dunia .”Tumepoteza hali ya kutafakari; tunapaswa kurejea nyuma, amesema.

Kuwajali masikini

Papa amesisistiza kuwa wakati huu wakati wa dunia wanapaswa kutafakari zaidi kuhusu maskini.

”Huu ni wakati wa kuwaangalia maskini.Yesu anasema tutakua na maskini wakati wote pamoja nasi, na ni kweli. Maskini ni ukweli ambao hatuwezi kuukataa,Lakini maskini wamefichwa,kwasababu umaskini ni aibu”.aliongeza.

Katika mji wa Roma hivi karibuni, wakati wa karantini, polisi alisema: Huwezi kuwa mtaani,nenda nyumbani.” Jibu lilikua : “Sina nyumba. Ninaishi mtaani.”

Kuna idadi kubwa ya watu wa aina hiyo ambao ni maskini. Nahatuwaoni kwasababu umaskini ni aibu. Wamekua ni sehemu ya ardhi; tunawaona kama vitu.

Mother Teresa aliwaona na akawa na ujasili wa kuanza safari tafakari. ”Kuwaona maskini inamaanisha kurejesha utu wao. Wao sio vitu, sio takataka ; ni watu” amesema Papa

Hatuwezi kuwa na sera za maisha bora ya watu sawa na za kuwanusuru wanyama, jinsi maskini wanavyotendewa mara kwa mara.

Papa amesema a kutoa ushauri na akasema huu ni wakati wa kwenda mashinani .

”Wafanyakazi wa hospitali ya gereza wamekua wakiwatumikisha vibaya wafungwa wao kama vitu. Na kuangalia jinsi wanavyomtendea Yule ambaye amekufa, hadi Yule ambaye amelala kitanda kilichopo karibu anawaambia : “Inatosha! Yeye pia alikua na mama!”, alilalamika Papa Francis.

Amesema tunahitaji kujiambia mara kwa mara: ”Yule maskini alikua na mama ambaye alimlea kwa upendo. Baadae maishani hatujui ni nini kilichotokea. Lakini inasaidia kufikiriakuwa upendo ambao alipata wakati mmoja kupitia mama yake kwa matumaini”.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki amesema dunia inawanyima uwezo maskini . ”Hatuwapi haki ya kuwaota mama zao. Wengi wanaishi kwa mihadarati. Na kuwatembelea inaweza kuleta thamani ya kiimani, inayoelekezwa kwa Mungu na kwa majirani zetu.

Wanaoumia kote duniani. Hii ndio tafakari tunayopaswa kufanya. Nendeni kote, na mfikishe habari njema kwa maskini .Na kama hatutaanzia hapa, basi hakutakua na mabadiliko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents