Burudani

Party Zone ya AY ni video na nusu, KALIIIIIIIII!

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=6NEeTyYEgsE’>Party Zone- AY[/youtube]

Wakati leo ni siku ambayo Ay ameelekea Afrika Kusini kuungana na bendi ya Sauti Sol kwa ajili ya show ya kesho kwenye Big Brother Africa, msanii huyo wa Tanzania mwenye mafanikio yasiyo na kifani ana kila haki ya kutabasamu muda wote.
Show hii imekuja muda muafaka wakati jana video yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kutoka rasmi.
Kwenye mitandao ya kijamii jana na siku nyingi zijazo video hii imezungumzwa/itazungumzwa sana na wapenzi wa muziki nchini na kwingineko.
Tunathubutu kusema kuwa hakuna video ya msanii wa Tanzania iliyowahi kutoka ukaifananisha na video ya Party Zone.
Hii ni video kali asikuambie mtu! Ni halali ilipiwe zaidi ya shilingi milioni 30. Ni aina ya zile video ambazo tumekuwa tukiziona sana Channel O ama MTV Base halafu tukaanza kujiuliza “Kwanini wabongo hatuna video kama hizi?”
Si uzuri wa video tu ndo utakaokupa raha ya kuangalia bali wimbo wenyewe pia. Jamaa wamepiga penyewe! Muziki wa aina hi indo upo kwenye soko sasa. Electronic dance na aina ya nyimbo kama hizo ambazo zilianza kuwa maarufu sana barani Ulaya zimekuwa maarufu mno miaka miwili iliyopita kiasi cha kuwafanya wasanii wa Marekani pia kama Usher, Chris Brown, Rihanna na wengine kuzifanya sana.
Pamoja na kwamba milango ya kimataifa ilikuwa imefunguka kitambo kwa Ay, tutegemee mambo makubwa zaidi kutokana na wimbo huu. Wimbo huu utampa nominations kibao za tuzo za kimataifa na kama Mungu akiwa upande wake tunaamini atakuwa nazo nyingi za kuweka kwenye kabati yake mwaka huu na ujao.
Wanamuziki wenzie wameikubali pia video yake. Hawa ni miongoni mwao na kile walichosema:
Miss Triniti: New video a gwaan. More Success to you mi fren!
WyreDaLoveChild: Great new video bro! You never stop setting the pace! Jah Bless.
Hamis Mwinjuma aka MwanaFA: Hii video ukiikataa utakuwa unajifunza uchawi tu!sikuskizi!HAKUNA video ya kiwango hiki Bongo..yes i said it,HAKUNA #partyzone!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents