Bongo Movie

Pastor Myamba azungumzia malengo ya chuo chake cha uigizaji filamu

Emmanuel Myamba akitoa maelekezo kwa wanafunzi wake

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Emmanuel Myamba maarufu kama Pastor Muyamba amesema aliamua kufungua chuo cha uigizaji ili kufanikisha kuifanya tasnia ya inafanikiwa na kusonga mbele zaidi.

‘Kutokana na tasnia ya filamu ilivyo nikaamua kufungua chuo ili kuepuka kuokotanaokotana mtaani inakuwa inaleta usumbufu kwasababu unakuwa unaanza kuwafundisha upya na kusababisha kupoteza muda, Myamba aliiambia Bongo5 ilipomtembelea chuoni kwake.

Wanafunzi wakiwa darasani

“Hiki chuo nilichofungua kitakuwa kinatoa taaluma ambayo inalingana na vyuo vyote kutokana walimu ni professional kutoka vyuo vikuu kwahiyo natarajia taaluma ya uigizaji wa filamu itasonga mbele kutokana na wahitimu watakuwa ni wenye kufahamu nini wanatakiwa wafanye katika jamii hii. Mimi sifundishi kwasababu siyo mwalimu ila ninatumia uzoefu wangu kwa kuwaelewesha nini wanatakiwa wafanye nikiwa kama ni mwigizaji wa muda mrefu kwahiyo panapo itajika kuwaelekeza nini wanatakiwa wafanye nawaelekeza.”

Kuhusu ujio wa kazi zake mpya, Myamba amesema, “naomba wadau wasubiri kazi zangu mbili ambazo ni GOD’S KINGDOM na MY MAN ambazo zitakuwa na ubuniifu wa hali ya juu na God’s Kingdom nitakuwa na wasanii wengi wenye majina makubwa kama Pancho Mwamba na Jengua na wengine wengi ambao watakuwa wamebeba uhusika kisawa sawa kwahiyo wadau wangu wasubiri vitu vizuri ambavyo vitakuwa vimebeba ujumbe mzuri wa kimaadili ambao utakuwa unaelimisha , kuburudisha, kuonya na kutoa taarifa kwa jamii kuhusu mambo mbali mbali.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents