Shinda na SIM Account

Pata mashairi ya wimbo wa Yalaiti

mwana_fa
Baada ya watu wengi wakijikuta wakiupenda wimbo wa Yalaiti, wa Mwana Fa na Linah, Bongo5 imeamua wimbo huo kuuchukua na kuuleta kwenu. Haya ni mashaili ambayo yanapatikana kwenye wimbo huo, ambao kwa sasa unafanya vizuri sana.

 

Wimbo; Yalaiti

Mwimbaji; Mwana Fa Feat Linah

Studio; Mj Record

Producer; Marco Chali

Sshhhh,classic classic..
Keeping the good music alive,
That’s me job,
You my sunshine my moonlight and everything I dream about,
Linah,let’s go..

Chorus..
Yalaiti,napenda pasi kifani/
Tofauti,sikutilii moyoni/
Sikuachi,leo na kesho peponi/
Anh anh anh anh anh anh I love you/

Verse I
Sambaza love kama dawa/
huachi mpaka napagawa/
hata ukisema mi sio Hamis natingisha kichwa/
mapenzi yako yanielemea ka chupa nzima ya tequila/
usirushe somo nakupenda acha masihara/
ina haja gani unishikie fimbo ili nikuskize ka gorilla/
mi ni mtu na mapenzi yangu nishaacha zamani usela/
una matatizo najua,na mi nna yangu boo/
we sit together from this moment,we see them through/
nikikukosea nisute,nipige vibao,nizodoe/
ninunie kwa siku kadhaa ila nnachoomba usinikimbie/
mapenzi ya utemi kwangu hadithi mambo ya kizamani hayo/
ukiniudhi ntapiga kwa khanga ndio nimefunzwa Tanga hivyo/
utaoga mabusu nikufute kwa kumbatio/mpaka kama nikisafiri ukinikumbuka iwe kilio/
sipendi mapenzi napenda mapenzi nawe/
usinikatae utaniumiza mi nna biashara na wewe/B…
Chorus..

Verse II
Nshasema sipendi mapenzi napenda mapenzi nawe/
usinikatae utaniumiza mi nna biashara na wewe/
ushaangaliwa niunge tela usingoje mpaka uambiwe/
ushaangukiwa anguka nawe usizubae mpaka irejewe/
kwako ntakuwa Bushoke sitajiuliza ka zezeta/
yetu yawe mahaba mapenzi zamani tumepita/
mi sakafuni we ukingoni mbio zangu haziendi mbali/
una moyo wangu ntapenda bila kujali/hata marefa wana timu zao mama panga matokeo/
pambano lianze najua goli ngapi ngapi leo/
usiache kuvaa nguo ndefu hivi vimini achia vicheche/
mwanamke kwetu staha tunaovipenda sio wote/
akili haziuwezi moyo na wenyewe una ubongo pia/
hauwezi ukafuatafuata kila utakachouambia/
nitajiwapo mapenzi naipata picha yako kwanza/
natamani uipate yangu na iwe inakuliwaza/

Linah..
Toa shaka na wasiwasi moyoni/
Toa shaka na wasiwasi moyoni/
Kukuepuka hilo haliwezekani/
Takushika,leo na kesho peponi/

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW