Aisee DSTV!

Pato la Mtanzania laongezeka kwa Tsh 100,000/=, Uchumi wa nchi wakua, Serikali yaeleza sababu (+video)

Serikali kupitia Wizara ya Fedha imesema kuwa pato la wastani la kila Mtanzania lilifikia Tsh. milioni 2.4 mwishoni mwa mwaka jana kutoka Tsh Milioni 2.3 mwaka 2017.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango  leo Juni 13, 2019 bungeni wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020.

Dkt. Mpango amesema ongezeko hilo ni sawa na wastani wa 5.6%, Ambapo kutokana na takwimu hizo ongezeko hilo ni sawa na Tsh 100,000/= kwa kila Mtanzania.

Kwa upande mwingine, Waziri mpango amesema kuwa pato la Taifa limekua kwa asilimia 7.0 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 kwa mwaka 2017.

Akitaja sababu za pato la Taifa kukua, Dkt. Mpango amesema kuwa ni kuongezeka kwa uwekezaji katika miundombinu kama ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya ndege.

Sababu nyingine ni kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme, kuimarika kwa huduma za usafirishaji na hali nzuri ya hewa iliyopelekea uzalishaji mzuri wa chakula na mazao mengine ya kilimo.

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW