Burudani

Patoranking wa Nigeria ashinda tuzo iliyokuwa ikiwaniwa na Diamond kwenye ‘2015 Ghana Music Awards’

Muimbaji wa dancehall Patoranking kutoka Nigeria ambaye mwaka jana (2014) alikuwa miongoni mwa wasanii wa kimataifa waliotumbuiza kwenye tamasha la Fiesta jijini Dar, ametajwa kuwa mshindi wa kipengele cha Msanii Bora wa Afrika wa mwaka kwenye tuzo za ‘2015 Vodaphone Ghana Music Awards’ (VGMA).

Patpranking

Tuzo hizo zimetolewa Jumamosi April 11, 2015 kwenye ukumbi wa Accra International Conference Centre (AICC) nchini Ghana.

Diamond Platnumz ndiye aliyekuwa akiiwakilisha Tanzania kwenye tuzo hizo katika kipengele cha ‘African Artiste of the Year’.

Wasanii wengine waliokuwa wakiwania kipengele hicho ni AKA (South Africa), Tiwa Savage (Nigeria), Yemi Alade (Nigeria) na Mavins (Nigeria).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents