Michezo

Patrick Phiri awa kocha mpya wa Simba SC

Klabu kubwa na ya muda mrefu nchini, Simba SC imepata kocha mpya, Mzambia, Patrick Phiri aliyewasili August 13 kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam mchana tayari kwa kusaini mkataba wa kurithi mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic aliyetimuliwa mwishoni mwa wiki.

Philli
Kocha Phiri alipokewa kwa mashada ya maua

Phiri ni kocha anayependwa sana na mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo hasa kwa rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.

August 14 anatarajiwa kusaini mkataba wa kuifundisha klabu yake hiyo ya zamani, Simba SC.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents