Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Paul Kagame azidi kung’ara kimataifa, sasa atawawakilisha marais wote wa Afrika kwenye ufunguzi wa Kombe la Dunia

Rais wa Rwanda, Paul Kagame ndiye rais pekee kutoka bara la Afrika atakayewawakilisha marais wote kwenye sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia nchini Urusi.


Paul Kagame na Vladimir Putin
Kagame ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mapema jana alikutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin katika Ikulu ya nchi hiyo na kufanya mazungumzo naye.

Hata hivyo, bado haijatajwa kama atapata wasaa wa kutoa hotuba fupi katika sherehe hizo za ufunguzi wa kombe la Dunia ambazo zinatarajiwa kufanyika jioni ya leo.

Mwezi uliopita Rais Kagame alifanikiwa kuitangaza kimataifa nchi yake hususani kwenye sekta ya utalii baada ya taifa hilo kuingia makubaliano ya kibiashara na klabu ya Arsenal.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW