AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Paul Pogba aja na style mpya ya nywele (+video)

Nyota wa Manchester United, Paul Pogba ameposti video yake inayomuonyesha akitengeneza ‘style’ mpya ya nywele zake ikiwa imesalia siku moja pekee kabla ya kuingia uwanjani kuikabili timu ya Leicester City.

Pogba ambaye ameisumbua United siku za hivi karibuni juu ya swala lakuihama timu hiyo na kuelekea nchini Hispania La Liga kujiunga Barca imekuwa ni kawaida kwake kutengeneza nywele zake kila msimu.

Mshindi huyo wa kombe la Dunia kupitia timu yake ya taifa ya Ufaransa ameposti kipande cha video kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram huku ikimuonyesha akinyolewa na kuchorwa alama ya nyota mbili ambazo mwenyewe anamaanisha idadi ya makombe ya dunia waliyochukua timu ya Ufaransa.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW