Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Paul Pogba ajitoa kwenye mbio za kuwania Ballon d’Or ‘Hapana mimi sistahili tuzo hii’

Kiuongo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba amesema kuwa hastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or  na hivyo kuonekana kama anajitoa mwenyewe bila hata kuondolewa kutokana na idadi ya kura zitakazopatikana baada ya kupigwa.

Pogba ni miongoni mwa majina 30 yaliyotajwa kwenye listi ya kuwania tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia ambayo inatarajiwa kutolewa jijini Paris Desemba 3 mwaka huu.

Kiungo huyo amesema kuwa angependa kuona wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ufaransa wakichukua tuzo hiyo ila yeye anaona hastahili.

Kuna jumla ya wachezaji saba wa timu hiyo ya Ufaransa waliyotajwa kwenye orodha ya watu 30 wanaowania Ballon d’Or akiwemo kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante na mlinda lango wa Tottenham, Hugo Lloris wengine ni Kylian Mbappe wa Paris Saint-Germain, Antoine Griezmann anaekipiga Atletico Madrid, Raphael Varane wa Real Madrid na Karim Benzema.

“Pengine anaweza kuwa Grizou (Griezmann), Kylian (Mbappe) au Raph’ (Varane), hawa wanastahili zaidi kuliko hata mimi,” Pogba ameiambia AFP.

Pogba ameongeza “Mimi si miongoni mwa wanaostahili hili. Lakini matumaini yangu yote yapo kwa hawa wachezaji watatu na pengine wanne ni NG (Kante).”

Tangu mwaka 2018 imekuwa ni Messi na Cristiano Ronaldo pekee ndiyo wanaochukua tuzo hii ya Ballon d’Or na hata mwaka huu wawili hawa majina yao yamejitokeza tena kwenye listi hiyo ya watu 30.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW