Uncategorized

Paul Pogba akiri jambo hili kwa maskitiko ‘Tumevunja heshima ya timu’

Kiungo wa Mchester United, Paul Pogba akiwa kwenye muonekano wa maskitiko amesema kuwa matokeo ya kipigo cha mabao 4 – 0 kutoka Everto ni kuishushia heshima klabu hiyo.

Siku ya Jumapili Manchester United ilikubali kipigo cha aibu cha mabao 4 – 0 kutoka kwa Everton mchezo wa Premier League hali iliyopelekea kufifisha matumaini ya timu hiyo kuingia kwenye nafasi nne za juu ili kupata fursa ya kushiriki Champions League.

Akizungumzia matokeo waliyopata dhidi ya Everton mchezaji huyo raia wa Ufaransa amesema “Kwa namna tulivyocheza, na uwezo tuliouonyesha kama timu, kila mmoja wetu tumejivunjia heshima.”

Paul Pogba ameongeza “Tumeshindwa kujiheshimu hata sisi wenyewe, klabu au washabiki wetu. Kila kitu kimekwenda hovyo.”

“Tumemwacha kocha ameongea, benchi limezungumza kwenye chumba cha kubadilishia nguo na waliongea ukweli. Wamesema kile kilichotokea kwenye mechi na hii sio heshima kwetu kwa kile tulichofanya uwanjani, sio heshima hata kwa wachezaji wenzetu, kwa mwenyekiti na wafanyakazi na watu wote.”

Pogba amesajiliwa akitokea klabu ya Juventus mwezi Agosti mwaka 2016 kwa mkataba wa miaka mitano, amekuwa akihitaji na Barcelona hali iliyopelekea wengi kuamini angeondoka kipindi cha kiangazi kwa matokeo ya juzi yanawafanya watu kufikiria kuwa wachezaji hao wameshindwa kuipa heshima timu hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents