Tupo Nawe

Paul Pogba aliendeleza bifu lake na Mourinho, amjibu kwa staili hii

Sihitaji kuwa Nahodha

Paul Pogba amesema kuwa hahitaji kuvaa kitambaa cha nahodha ili kuwa kiongozi wa wachezaji. Kauli hiyo ya Pogba ambaye ni kiungo mchezeshaji wa klabu ya Manchester United inachukuliwa na wadadisi wa soka kama ni kijembe kwa kocha wake, Jose Mourinho.

Pogba alivuliwa na Mourinho cheo cha nahodha msaidizi wa klabu hiyo mwezi uliopita. Hatua hiyo ilifuatiwa na kitendo cha mchezaji huyo kukashifu hadharani mbinu za kocha wake.

Pogba alikuwa akimsaidia Ashley Young majukumu ya unahodha katika kipindi hiki ambacho nahodha Antonio Valencia hayupo.

Kiungo huyo yupo kambini na kikosi cha timu yake ya taifa ya Ufaransa na alitoa kauli hiyo alipoulizwa kama anaona uwezekano wa kuwa nahodha wa taifa lake katika siku za usoni.

“Sijawahi kulitumikia taifa langu ili niwe nahodha. Kuwa hapa pekee ni kitu kikubwa sana kwangu,” amesema na kuongeza: “Si lazima uwe nahodha ndio uongee, kiongozi si mtu mwenye kitambaa.Kama kiongozi utaongea kwenye uwanja, lakini nimeona viongozi wasiooongea pia.” Pogba amejinasibu kuwa yeye ndio mtu sahihi kwa kuwaunganisha wachezaji wadogo na wakubwa ndani ya kikosi.

“Kwa umri wangu wa miaka 25, nipo katikati ya wachezaji wadogo na wakubwa kiumri. Hali hiyo inanipa wasaa wa kufikisha ujumbe kwa pande zote na kusikilizwa,” amesema Pogba.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW