Aisee DSTV!
SwahiliFix

Paul Pogba atembelea Mecca na kuandika ujumbe huu ‘Kamwe usisahau vitu muhimu katika maisha’

Nyota wa Manchester United, Paul Pogba amewasili mji mtakatifu kwa imani ya dini ya Kiislam wa Mecca (Maka) katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ameonekana akiwa karibu kabisa na al-Ka bah ambayo ipo kwenye nchi ya Saudi Arabia mara baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu.

Hii si mara ya kwanza kwa mfaransa huyo kutembelea mji huo mtakatifu alishawahi kufanya hivyo katika misimu miwili iliyopita.

Kupitia akaunti yake ya kijamii ya instagram, Pogba ameposti picha zake akiwa Mecca (Maka) huku akiandika ujumbe kuwa kamwe usisahau vitu muhimu katika maisha. ”Kamwe usisaha vitu muhimu katika maisa”.

Pogba alipitia wakati mgumu sana wakati timu yake ilipokubali kipigo cha mabao 2 – o dhidi ya Cardiff kwenye mchezo wake wa mwisho wa ligi pale Old Trafford.

Ambapo alikubali kupokea matusi kutoka kwa mashabiki wa Manchester United mwishoni mwa wikiend kutokana na matokeo hayo. Hata hivyo, Pogba anahusishwa kutimkia Real Madrid kutokana na meneja wa klabu hiyo  Zinedine Zidane kuhitaji kumsajili.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW