Michezo

Paul Pogba ‘Man of the Match’ Vs FC Basel

Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Labile Pogba amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa hapo jana dhidi ya FC Basel katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Labile Pogba

Katika mchezo huo wa kundi A, United ilikubali kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wao timu ya Basel lililofungwa na mchezaji Michael Lang dakika ya 89 kunako dimba la St. Jakob-Park.

Beki wa Basel, Michael Lang akishangiria baada ya kuifunga Manchester United

Kwa matokeo hayo inaifanya Man United kuwa katika hali mbaya kutokana na msimamo wa kundi hilo kuanza kuwa mgumu dhidi yake na hivyo italazimika kupambana kufa na kupona ili kuhakikisha inachomoza na uishindi dhidi ya CSKA Moscow wakati wapinzani wake wakaribu Basel itakapowafuata vibonde Benfica.

Mfumo wa kucheza kwa kujilinda ‘kupaki basi’ ndiyo uliyowagharimu zaidi United katika mchezo wa hapo jana usiku hivyo watalazimika kushambulia zaidi ili kupata nafasi ya kuingia hatua ya 16 bora.

Msimamo wa kundi hilo kwa sasa Manchester United ina pointi 12, FC Basel ina alama 9, CSKA Moscow 9 na Benfica pointi 0.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents