Michezo

Paul Scholes amjia juu Mourinho baada ya matokeo na Valencia kwa kusema haya

Paul Scholes amjia juu Mourinho baada ya matokeo na Valencia kwa kusema haya

Wachezaji wengi wa ambao waliwahi kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Old Trafford jijini Manchester,wamekuwa wakitoa ushauri wao kwa makocha wengi ambao wamefanikiwa kuitumikia klabu hiyo baada ya kustaafu Sir Alex Ferguson.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakiwashauri sana mameneja wa klabu hiyo ni Gary Neville,Phil Neville,Ferdinand,Paul Scholes na wengineo,katika kipindi cha hivi karibu timu hiyo ilimpata kocha mwingine ambaye ni Mreno Jose Mourinho.

Kocha huyo kwa kipindi kirefu alianza kujiita special one kutokana na mafanikio yake katika baadhi ya vilabu alivyovifundidha huku vilabu hivyo vikipata mafanikio kutokana kufanya vizuri.

Miongoni mwa vilabu alivyowahi kuvifundisha ni pamoja na Porto,Chelsea,Intermilan,Real Madrid pamoja na Manchester United lakini katika klabu mbili ambazo Mreno huyo hajawahi kuviletea mafanikio ni Real Madrid na Manchester United,

Licha ya kutokupata mafanikio kwenye vilabu hivyo,hali yake imekuwa mbaya zaidi katika klabu ya Manchester United,kocha huyo aliisaidia timu hiyo kufanya vizuri msimu uliopita kwa kuisaidi kuweza kuwa ni miongoni mwa vilabu vinne bora katika ligi kuu nchini humo

Baada ya kuanza msimu huu klabu hiyo imeonekana kufanya vibaya kwani hadi sasa imecheza michezo 7  ikishinda michezo mitatu ikipata sare mchezo moja na kupoteza michezo mitatu,ikiwa na alama 10 na ikiwa nafsi ya 10.

Kwa matokeo hayo ambaye timu hiyo inaendelea kuyapata yameacha maswali mengi sana kwa wadau mbalimbali wa soka duniani,licha ya kupoteza michezo mitatu ya ligi lakini hadi hivi sasa timu hiyo haijapata ushindi katika michezo minne mfululizo katika michuano yote.

Baada ya mchezo wao dhidi ya Valencia katika uwanja wa Old Trafford wakiitumikia michuano ya UEFA Champions League,timu hiyo ilishindwa kupata matokeo chanya katika uwanja wa nyumbani kwa kulazimishwa sare tasa ya bila kufungana huku wakihudhuria wakongwe wengi waliowahi kuitumikia klabu hiyo miaka ya nyuma,na baada ya matokeo hayo wamejitokeza wadau wengi sana na kukiponda kiwango cha timu hiyo kikubwa zaidi wakiuponda mfumo wa kocha wa timu hiyo.

Lcha ya kukiponda kiwango cha Mourinho lakini pia kipindi cha nyuma mchezaji wa United na taifa la Ufaransa Paul Pogba aliwahi kusema kuwa wanahitaji kushambulia wakiwa nyumbani,na alipoulizwa kkwanini sasa hawashambuliia akajibu hajui na aulizwe kocha, hayo maneno yalimuumiza kwa kiasi fulani kocha huyo na kuanzia hapo aliamua kumnya’anya hadhi ya Unahodha msaidizi na kuwa mchezaji wa kawaida.

Baada ya mchezo wa jana mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Paul Scholes aliweza kuzungumza na kusema kuwa ” Kiwango cha Mourinho kimefikia mwisho na matokeo wanayoendelea kuyapata ni ya aibu kabisa”

By Ally Juma

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents