Videos

Paul Walker, Heath Ledger, Brandon Lee walipoteza maisha wakati wakiendelea kushoot filamu mpya

Kipindi Paul Walker alipouawa kwenye ajali mbaya ya gari huko Santa Clarita, California Jumamosi iliyopita, alikuwa kwenye mapumziko mafupi kutoka Atlanta ambako alikuwa akishoot filamu ya Fast & Furious 7.

paul-walker-uk-premiere-fast-and-furious-6-01
Paul Walker

Bado muongozaji wa filamu hiyo James Wan au Universal Pictures hawajatoa maelezo ya kutosha kuhusu namna gani kifo cha Walker kilivyoathiri filamu hiyo japo kazi itaendelea.

Kumekuwepo pia filamu zingine kubwa zilizoathirika na kifo cha ghafla cha muigizaji wake mkubwa. Nyingi ziliandikwa upya na kuhaririwa kwa umakini. Hawa ni waigizaji wengine waliofariki wakati wakiendelea kushoot filamu kubwa.

Heath Ledger – The Imaginarium of Doctor Parnassus
Heath-heath-ledger-31421105-576-853

Mwanzoni muongozaji wake Terry Gilliam alidhani asingeweza kuimalizia filamu hiyo, The Imaginarium of Doctor Parnassus kufuatia kifo cha muigizaje wake mkuu January 2008 Heath Ledger. Utengenezaji ulisimama kwa takriban mwezi mmoja kabla ya kuamua kuendelea na waigizaji wengine Colin Farrell, Jude Law, na Johnny Depp kucheza sehemu za Ledger.

http://www.youtube.com/watch?v=6jU3AimFaz0

Brandon Lee – The Crow

00/02/1991. STUDIO: BRANDON LEE

Pale Brandon Lee alipopigwa risasi na kufa kimakosa wakati akishoot filamu ya The Crow, Paramount Pictures iliamua kutoitoa. Miramax iliichukua na kuongeza bajeti ya dola milioni 8. Baada ya mapumziko ya kuiandaa tena, The Crow ilikamilika na kuwa na mafanikio makubwa. Sehemu aliyopigwa risasi Lee haikuwekwa kwenye filamu.

http://www.youtube.com/watch?v=xO1K_xS6HNU

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents