Pawpaw wa Nollywood ala shavu la zaidi ya tsh mil.100 nchini Afrika Kusini

Ni shangwe tu kwa muigizaji maarufu wa Nollywood Osita Iheme maarufu sana kama Pawpaw kwakuwa amekamata mchongo wa nguvu nchini Afrika Kusini.

Vyanzo vya nchini Nigeria vimesema kuwa muigizaji huyo mwenye umbo dogo na kipenzi cha watoto alikuwa nchini humo kuangusha wino kusaini mkataba huo.

Deal hiyo itamfanya Pawpaw kuwa sura ya kituo cha runinga cha burudani cha nchini humo VUZU TV.

Mchongo huo ambao kwanza utakuwa wa miezi sita na huenda ukaongezewa muda umempa mezani kiasi cha naira milioni 11 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100 za Tanzania.

Umaarufu wa Pawpaw ulianza kusambaa baada ya kuigiza filamu maarufu ikiwemo ‘Aki Nakwa’ ambayo aliigiza na Aki, ambaye ni kama pacha wake wa kwenye filamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents