Habari

Paypal yamtajirisha mwanaume wa Marekani na kumfanya ‘QUADRILLIONAIRE’ kwa bahati mbaya ila………!

Mteja wa huduma ya Paypal Chris Reynolds amejikuta anapigwa na butwaa kwa mshangao baada ya kukuta kiasi kikubwa sana katika akaunti yake ya kampuni ya kutuma na kupokea pesa mtandaoni ‘PayPal’.

pay pol

Reynolds mwenye miaka 56, baada ya kuangalia salio la akaunti yake ndipo alipokutana na salio ambalo lingemfanya kuwa ‘QUADRILLIONAIRE’ na mwanaume mwenye pesa nyingi zaidi duniani.

Ijumaa iliyopita Mr Reynolds, kutoka Delaware Marekani, wakati anaangalia taarifa ya kila mwezi ya akaunti yake ya Paypal kwa barua pepe ndipo alipogundua salio lake lilikuwa linasomeka $ 92.233.720.368.547.800.

Akiwa bado amepigwa butwaa kwa mshangao Reynolds aliamua kuingia kwenye mtandao wa Paypal ili kuthibitisha salio aliloliona katika email yake, ndipo ndoto yake ilifikia ukingoni baada ya kulog katika akaunti yake na kukutana na salio “0”.

Pamoja na jamaa huyo kujua kuna kosa lilifanyika kwenye taarifa ya mwezi ya akaunti yake aliyotumiwa katika barua pepe lakini aliamua kuendelea kuota mchana kweupe na hivi ndivyo alivyokuwa anapanga kuzitumia pesa hizo ‘za ndotoni’:

1. Kwanza kabisa angelipa deni la Marekani kama ilivyoripotiwa na mtandao wa Philly.com “I’m a very responsible guy. I would pay the national debt down first.” alisema LOL!!!

2. Pili alisema angeinunua timu ya baseball ya Philadelphia Phillies

Hata hivyo msemaji wa Pay Pal alisema kampuni yao huwa haijadili taarifa za akaunti za wateja wao, pale alipotakiwa kuelezea tukio hilo.

SOURCE: DAILY MAIL

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents