Burudani

Penzi la 21 Savage lampagawisha Amber Rose, aanza kutoa mwenyewe

Utatoa utoi? Mapenzi ya Amber Rose kwa mpenzi wake rapper 21 Savage si mchezo. Mwanamitindo huyo anadaiwa kumnunulia mpenzi wake huyo pete ya ishara ya uaminifu kwake ambayo imeandikwa kwa jina la “Loyality 21.”

Kwa mujibu wa sonara Ben Baller ambaye ametengeneza pete hiyo, kupitia mtandao wa Instagram amesema, mawe takribani 1,100 ametumia kuitengeneza pete hiyo ikiwemo dhahabu nyeupe, almasi a aina ningine ya madini.

“Custom made 18K White Gold Promise Eternity Ring. 7 Carats of Internally Flawless F Color Round Brilliant White Diamonds with “LOYALTY 21″ spelled out in Natural AAA Red Rubies. 1100 stones total. Commissioned by @amberrose made for @21savage #IFANDCO ?❤️?,” ameandika Ben kwenye video aliyoiweka katika mtandao huo akiionyesha pete hiyo.

Pete hiyo ameonekana Savage ameivaa usiku wa Jumapili iliyopita katika utoaji wa tuzo za MTV Video Music Awards zilizofanyika mjini California.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents