DStv Inogilee!

Penzi la Khloe Kardashian na Tristan Thompson laota mbawa, mmoja amsaliti mwenzie kwa shemeji yake

Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho na hili linadhirika kwa wawili wapendanao, Khloe Kardashian na mpenzi wake Tristan Thompson ambao wamemwagana kwa kisa cha usaliti.

Image result for khloe kardashian and thompson
Khloe na Thompson

Kwa mujibu wa mtandao wa E-News, umeeleza kuwa Khloe ameachana na mzazi mwenzie kwa tuhuma za usaliti.

Thompson ambaye ni mchezaji wa kikapu katika klabu ya Cleveland Cavaliers. Imeelezwa kuwa siku ya wapendanao Februari 14 mwaka huu alitoka na familia yake mjini Los Angeles na baadae Jumapili akiwa bado mjini humo alienda klabu na rafiki yake na mrembo Kylie Jenner aitwaye Jordyn Woods ambapo huko ndio usaliti ulifanyika.

Wawili hao wamefanikiwa kupata mtoto mmoja na wamekuwa kwenye migogoro ya kifamilia tangu mwaka 2017.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW