Burudani

Penzi la Wema Sepetu lachanua upya, Diamond atajwa

Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika. Malkia wa filamu nchini Tanzania Wema Sepetu Jumatatu hii amepost picha ya ua la rose “Red Rose’ ambalo linadaiwa kuwa ni ishara ya upendo.

Mwigizaji huyo amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuweka wazi mahusiano yake toka aachane na mchekeshaji Idris Sultan kitu ambacho siyo kawaida yake katika maisha yake.

Jumatatu hii amepost ua jekundu ikiwa ni ishara ya upendo huku akiandika ujumbe unaosomeka ‘A Red Rose is a Symbol of Love…’.

Hatua hiyo imechukuliwa tofauti na mashabiki wengi wa mrembo huyo baada ya hivi karibuni kuonekana kuwa karibu zaidi na mpenzi wake wa zamani, Diamond Platnumz.

Mashabiki hao wengi kupitia Instagram muda mchache baada ya mrembo kupost ua, amekuwa wakimtania kwa kusema kwamba huwenda mrembo huyo ameamua kurudia na Diamond ambaye ameachana na mama watoto wake, Zari The Boss Lady.

Maoni na mashabiki hao kupitia instagram.

udankimario

Madame wema nahisi kwa upande wa pili itakua ni Special kwa A boy From Tandale yan Simba😂😂

safiii_denis

Woyoooooooo kwetu raha siye twapost jekundu rose rose rose rose rose una rangi nyingi weweeeeee.

fatmarain39

Unahashuo wewe kwakuwa mwenzio kaweka black rose na wewe unatuekea red rose ovyoo

milly_ivan

Hatupendi black roses tunapenda red roses 😅😅😅 madam @wemasepetu

suleshcleverboytz

Jamanii Jamanii @wemasepetu kwan wamekukosea nini hawa watu @zarithebosslady@hamisamobetto @tundathebossbabemana huku Kunakoenda asaiv Vita Ya tatu Inaenda Kutokea SOOON 😂😂😂

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents