Michezo

Pep Guardiola amjibu Ronaldo baada ya kuitupa nje Benifica

Baada ya ndoto za Cristiano Ronaldo za kucheza na Benifica kwenye hatua ya nusu fainali ya Uefa kuzimwa na Bayern Munich, Guardiola amemjibu.

pep-guardiola-cropped_67ltmpxb078015dpu48guo5ak

Ni baada Cristiano Ronaldo kusema kuwa ana matumaini timu ya Benifica itaifunga Bayern kwenye hatua ya robo. Mechi ya jana usiku iligeuka na timu hizo zilitoka sare ya 2-2 na Bayern wakapita kwenye hatua inayofuata kwa jumla ya magoli matatu na Benifika wakiwa na magoli yao mawili.

Kutokana na kauli aliyoisema Ronaldo hapo nyuma, kocha wa Bayern, Pep Guardiola amesema, “I know that Cristiano would have liked Benfica in the semi-finals, I am sorry for him.”

“According to what I have read in Germany, if we do not win the Champions League my work will be incomplete in fans’ eyes,” aliongezea Pep.

Droo ya Uefa hatua ya nusu fainali itachezeshwa siku ya Ijumaa (kesho), timu zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo ni Atletico Madrid, Bayern Munich, Manchester City na Real Madrid.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents