Burudani

Peter Msechu Akosoa Ushindi TPF5


Mshindi wa Tusker Project Fame kwa msimu wa nne Peter Msechu, jana alitoa maoni yake juu ya washindi waliopatikana juzi usiku katika fainali ya Tusker Project Fame msimu wa tano iliyofanyika jijini Nairobi Kenya ambapo mshiriki kutoka Kenya Ruth Matete aliibuka mshindi wa jumla na kulamba kitita cha shiling Milioni 5 za Kenya.
Akiongea na kituo kimoja cha Radio Peter Msechu alisema yeye kimsingi anamkubali mshindi wa kwanza Ruth lakini kwa mtazamo wake anaona kuna mambo ambayo anahisi hayakuwa sawa, hasa nafasi ya mshindi wa pili na ya tatu ambapo yeye anaona mshiriki Jackson kutoka Rwanda alikuwa anastahili kuwamo katika nafasi ya pili bora.
Tunamnukuu “ Mimi mzee najua namna mambo yanavyoenda kule ndani na kwa kuwa nimeshashiriki katika mashindano ya namna hiyo ninashangaa kuona mtu anayejua kuimba ipasavyo anawekwa chini kama nilivyosema aali nafikiri Jackson alistahili kupewa nafasi nzuri zaidi”.
Katika hatua nyingine wadau, mashabiki na wapenzi wengi wa shindano hilo kupitia mitandao ya kijamii walitofautiana na uamuzi wa majaji katika upangaji wao wa matokeo hasa hasa namba 2 na 3 ambazo watu wengi wanafikiri kwa mtazamo wao mshiriki Jackson wa Rwanda ameonewa kupewa namba 2

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents