Burudani

Peter Msechu na Baba Levo kuja na Tv Show

Wasanii wa muziki Bongo, Peter Msechu amefunguka mipango ya kuja na tv show kati yake na Baba Levo.

Peter Msechu ambaye amekuwa akitaniana na Baba Levo katika mitandao ya kijamii ameiambia Clouds Fm kuwa utani wao unaweza kuwa biashara kwa kuanzisha kipindi cha Comedy kwani wamekuwa wakishawishiwa kufanya hivyo ila bado wanatafakari hilo.

“Watu wengi wamekuja kutushauri kufanya comedy lakini kimsingi mimi na Baba Levo tumekuwa tunatafuta direction, unajua vinaanzishwa vikundi vingi vya comedy lakini watu wanafeli, unajua kufanya comedy ni maamuzi magumu,” amesema.

“Hakuna kitu kigumu kama kumwambia mtu njoo ucheke halafu hacheki itakuwa ni ishu  kubwa, tumefatwa na tv station nyingi sana hadi za Kenya lakini bado tunachakata, tunaangalia mtu sahihi ni nani,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents