Burudani

Peter Okoye wa P-Square aishangaa serikali ya Nigeria

Peter Okoye kutoka kundi la P-Square ameonekana kukerwa na maamuzi ya serikali yake ya Nigeria kwa wasanii.

Msanii huyo wiki hii kupitia mtandao wake wa Twitter ameamua kufunguka yake ya moyoni baada ya serikali ya nchi yao kutangaza kuwazuia wasanii wa muziki na waigizaji kushoot video nje ya nchi hiyo.

“And our Government been failing us since 1960 #SMH. Dear FG, for your information! All the Shame way una dey bring for dis our country na we dey entertainers dey cover una Nash! Ndi ala #SMH. Sometimes am ashamed to be called a Nigerian because this people? Tufia kwa?? Another Nationality Loading…… ?????????????????? #shame,” aliandika kwenye mtandao huo.

Hata hivyo inadaiwa kuwa msanii huyo alitakiwa kufika polisi baada ya kutoa maneno hayo. Jumamosi ya wiki iliyopita Waziri wa Habari na Utamaduni wa Nigeria, Lai Mohamed, alisema hali hiyo imezuia uwezeshaji wa wataalamu katika sekta hiyo na kudhoofisha maendeleo ya sekta na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents