Burudani

Petit Man afunguka ishu ya kuweka rehani passport yake ya kusafiria baa (Video)

Meneja wa wasanii na mdau mkubwa wa sanaa, Petit Man amefunguka kuzungumza kwa mara ya kwanza tetesi ambazo zilikuwa zinadai kwamba wameweka rehani passport yake ya kusafiria baa baada ya kudaiwa pesa.

Wiki hii Bongo5 ilifanya mazungumzo na Petit ambapo alikanusha uvumi huo huku akidai kuna wabaya wake ambao walikuwa wanasambaza taarifa hizo za uongo.

“Sijawahi kufanya kitu hicho ndio maana hata sikuwahi kukizungumzia kwa sababu hates wako wengi sana, kuna watu wengi wanachuki na maisha yangu lakini sio habari za kweli na sijawahi hata kuitwa na Migration kwaajili ya hiyo ishu,” alisema Petit.

Mwezi mmoja uliopita Migration ya Tanzania ilitoa taarifa kwamba mtu yeyote ambaye atapoteza passport yake ya kusafiria atatiwa kulipa faini ya tsh 500000 ili apatiwe nyingine.

Walidai wamefikia hatua hiyo baada ya kugundua kuna baadhi ya watu wanaweka passport zao reheni kinyume na sheria ya Tanzania.

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents