Habari

Petit Man arudi Instagram na ujumbe ‘hatutaki mazoea kabisa’, mashabiki wampa pole

Mmoja kati ya watu 13 walioachiwa jana na mahakama kwenye sakata la Madawa ya kulevya, Petit Man amepost ujumbe wake wa kwanza katika mtandao wa Instagram huku akiweka sehemu ya wimbo wa msanii wake Billnass ‘hatutaki mazoea kabisa’.

Petit akwa mahakamani hapo jana na wenzake

Meneja huyo wa wasanii ndani ya label LFLG alikamatwa na jeshi la polisi mapema wiki iliyopita kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya pamoja na kutumia.

“Hatutakimazoeakabisa @billnass Feat @mwanafa #TurnOnComment #JahBless #LFLG,” aliandika meneja huyo Insta na kuleta mjadala mkubwa huku wengi wakimpa pole.

Petit Man, Said Alteza, Lulu Diva na wengine ambao walikuwa kwenye sakata hilo na kuachiwa na mahakama hapo jana, wametakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 20 na watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka mitatu. Iwapo watuhumiwa hao watashindwa kufuata masharti hayo watarudishwa tena mahakamani.

Huu ni ujumbe wa mashabiki hao wa Instagram.

nhappiness4

Toto nasikia ulipewa Mekong’oto wa haja hivi ni kweli da roho iliniuma kinoma

sherry_4real

Daah pole sn mshakaji wng ndo life ilivo cku azfanani kitu kidogo inaweza ikakuarbia siku au mwez pole sn dady yoo

florah_chiza
Welcome back petit hakika Allah amekupigania dady ake taraj

wemasepetu_habari_ya_mjini
Mpende Sana Mama Tarajii@_esmaplatnumz Nimeshuhudia Akihangaika Kwa Ajili Yako Jana Huyo Ndo Mwanamke Wako Mpende Sana Nawapenda????????????????????????@officialpetitman_wakuachetz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents