Habari
Pharrell Williams aachia video ya muziki yenye muda wa saa 24!!
Producer, rapper na muimbaji wa Marekani, Pharrell Williams, ameachia video ya muziki ndefu kuliko zote zilizowahi kufanyika. Video ya wimbo wake Happy ina muda wa saa 24, yes itakuchukua siku nzima kumaliza kuitazama.
Unadhani unaweza kuitazama yote? Una siku nzima ya kupoteza? Una bundle za kutosha basi bofya hapa kuitazama.
Kwenye video hii wameoneka mastaa wengine Steve Carrell, Janelle MonĂ¡e, Tyler The Creator, Kelly Osbourne na Pharrell mwenyewe.