Michezo

‘Philippe Coutinho’ achafua hali ya hewa Liverpool

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Liverpool Mbrazil, Philippe Coutinho amechafua hali ya hewa kwa mashabiki wa Liverpool baada ya kutamka wazi kuwa amezipata taarifa za kuhitajika na klabu ya Barcelona na yupo tayari kama ikitokea ofa.

Philippe Coutinho

Coutinho leo kwenye mahojiano yake na kituo cha Runinga cha ESPN Brazil, amesema amezipata taarifa za kuhitajika na Wababe hao wa La liga lakini kwa sasa anawaza zaidi kuitumikia Klabu yake ya Liverpool ili msimu ujao wacheze Klabu Bingwa barani Ulaya.

Countinho 24, ambaye jana ameisaidia Klabu ya Liverpool kuitwanga West Ham goli 4-0 huku akiwa na magoli 12 kwa msimu huu, aliyoifungia Klabu yake, amesema hakuna mchezaji ambaye anaweza kukataa kuchezea Klabu kubwa kama Barcelona hivyo amefurahishwa sana kuhusishwa na Klabu ya Barcelona.

Barcelona ni moja kati ya Klabu kubwa Duniani,Ingawaje mpaka sasa hivi sijapata taarifa yoyote kuhusu kutoka kwa Meneja wangu” amesema Countinho na kuendelea kusema

Nafurahi sana kusikia Klabu kubwa kama Barcelona inavutiwa na kiwango changu kwani inanipa nguvu sana uwanjani hakuna wakukataa kama ikitokea,Lakini kwa sasa akili yangu nimeilekeza kwenye timu yangu ili ifuzu kucheza michuano ya Klabu Bingwabarani Ulaya“Amesema Coutinho kwenye mahojiano yake na ESPN Brazil.

Kwa mujibu wa Gazeti la Marca taarifa zinasema Klabu ya Barcelona imetenga dau la Euro Milioni 70 kwa ajili ya kumnasa kiungo huyo.

Mashabiki wengi wa Liverpool wamekerwa na taarifa hizo hasa hasa mitandaoni wakisema kuwa timu yao imekuwa ikitengeneza tuu wachezaji bila kunufaika nao wakitolea mfano wa Luis Suarez ambae nae alihama klabuni hapo na kutimkia Barcelona.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents