Picha

Photos: Launch of Swahili Fashion Week 2012


It was an all glamour and glitz affair katika official Swahili Fashion week season 5 Launch Party, ambayo imezinduliwa rasmi jana usiku pale Thai Village Masaki jijini Dar Es Salaam…ambapo socialites, pamoja na party animals kibao walialikwa kushuhudia uzinduzi huo.
Akizindua Season mpya kwa mwaka huu wa 2012 mwanzilishi na mmiliki wa Swahili Fashion Week Mustafa Hassanali aliwashukuru wageni waalikwa, wadau, wadhamini na media kwa sapoti ambayo wamekuwa wakimpa katika season zote nne zilizopita. Mustafa alitaja baadhi ya vipengele ambavyo vitatengeneza season hii ya 5 ambapo aliesema kutakuwa na monyesho ya kazi za wabunifu (exhibition), (catwalk) onyesho lenyewe, mafunzo (workshop), na tuzo (awards) mbali mbali ambazo zitatolewa.

Mustaffa alianza kwa kutaja majina ya wabunifu wanaowania tuzo ya “mbunifu anayechipukia” ambapo wabunifu Neema Mnjama (Kenya), Neema Mtweve (Tanzania), Jackson Gumbala (Tanzania), Hilda Afanda (Kenya), Happyness Sosthenes (Tanzania), Naila Yusuph (Tanzania), Ally Salim (Tanzania), Catherine Mlowe (Tanzania), John Kapalata (Tanzania), Lilian Lawrence (Tanzania) na Philista Oniang’o (Kenya).

Aliwataja baadhi ya wabunifu ambao wataonyesha mavazi yao ambao ni pamoja na Ailinda sawe, Eskado Bird, Asia Idarous, Gabriel Mollel, Sarah Masenga, Martin Kadinda, Subira Mahure, Christina Zimba na Kemmy Kalikawe.

Alitaja tuzo zingine ambazo zitatolewa ni pamoja na tuzo ya Swahili Fashion Week Stylish Personality of the year ambayo ina vipengele viwili, moja ni kwa kina dada na kipengele kingine ni kwa kina kaka, ambapo Meya wa Ilala Jerry Silaa ni mmoja wa wanaowania tuzo hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa Swahili Fashion Week kumpata muwania tuzo ambaye ni High Ranking government official. Tuzo nyingine ni kwenda kwa Media Brands amabazo zimekuwa ziki sapoti Swahili Fashion week na media personality.
Baada ya maelezo hayo ilifuata ufunguzi rasmi wa party kwa wageni waalikwa kupata fursa ya kusakata muziki.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents