Picha

Xclusive Photos: Dar City Center Ilivyotisha

Mrembo Matilda Martin Jana usiku alitawazwa rasmi kuwa mshindi wa Miss Dar-Es-Salaam City Centre, baada ya kuwabwaga warembo wenzake 15 katika kinyang’anyiro cha kumsaka Redds Miss Tanzania 2012. Aliyeshika nafasi ya pili alikuwa mrembo Magdalena Munisi na watatu alikuwa mrembo Witness Michael, huku nafasi ya nne ikienda kwa Viola Mwamba na ya tano ikishikwa nae Laila Kheri.

Shindano hilo lilifanyika katika viwanja vya bustani ya hoteli ya kimataifa Golden Tulip iliyopo Masaki.Shughuli ilianza majira ya saa nne na robo usiku, ikiongozwa na Bendi ya Twanga Pepeta akiwemo Lwiza Mbutu, safu ya shoo ya wanenguaji wa kike pamoja na rapa machachari Msafiri Diof.

Baada ya Burudani hiyo alipanda stejini mkurugenzi wa Lino Iunternational Agency Hashim Lundenga na kumkaribisha mgenirasmi Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar-Es-Salaam Mama Sophia Mjema ambaye ni mkuu wa wilaya ya Temeke aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam,Said Melek, ambaye aliomba udhuru kwa kutingwa na shughuli nyingi nakutuma salamu zake.

Baada ya hapo washiriki walipanda stejini kufungua shoo kwa kucheza nyimbo mbili kwa ustadi wa hali ya juu, kitendo kilichoamsha nderemo na vifijo. Baada ya tukio hilo ilikuja awamu ya nguo za ubunifu ambapo washiriki walifika jukwaani na kujitambulisha kabla ya msanii wa kizazi kipya Rachel kupanda jukwaani na kutoa burudani kwa waliofika.

Aidha iliofuata vazi la Beach kabla ya vazi la Jioni ambapo mambo ndipo yalipoanza kunoga. Ilikuwa zamu ya washiriki kuulizwa maswali na mmoja ya majaji wa shindano hilo Wema Sepetu, ambaye kwa usiku wa jana aliacha gumzo la hali ya juu baada ya kupokelewa na mashabiki wake kwa vifijo na nderemo wakati wa kuitwa jukwaani.

Hatua ya maswali ndio ilifanya onyesho hilo la Miss Dar-Es-Salaam City Centre kuonekana linamsisimko. Hatua ya baadhi ya washiriki kutumia lugha ya kiingereza na kujieleza iligawa mashabiki kiasi cha kuwafanya majaji kuwa na kazi ya ziada wakati wa kutaja washindi wa tatu bora kwani kila raia aliyefika kwenye onyesho alikuwa na mshindi wake kiasi cha kuleta tafrani wakati wa kumtangaza mshindi ikionekana dhahiri kuwa watazamaji kwa ujumla wao walipinga matokeo kwa kuzomea kwa sauti ya juu.

Kituko kikubwa zaidi kilikuwa wakati msanii Diamond platnumz alipopanda stejini kutumbuiza na kuamsha chokochoko kati yake na wema Sepetu iliyokuwa imefikiriwa imeanza kupotea. Akiimba wimbo wa nimpende nani Diamond aliwateka mashabiki waliokuwemo ukumbini hasahasa wakina dada ambapo alipokuwa akiuliza kwenye korasi nimpende naniii? Ukumbi mzima ulilipuka kwa mayowe wemaaaaaaa hali iliyomletea taharuki kwa dada Wema ambaye alipata wakati mgumu kwa kipindi hicho cha burudani ya Diamond.
Yote kwa yote shoo ilikuwa nzuri na ilihudhuriwa na watu wengi wakiwemo mastaa kadhaa wa bongo wakiwemo kina Tunda Man, Sharo Milionea, Muzamir Katunzi, Bob Junior, Sheta, Ben Kinyaiya, Basila Mwanakuzi na wengineo wengi. Shughuli ilisherehekeshwa na Hamisi Mandi B12 na Sinta.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents