Burudani

Pic Of The Day: Ay na Jason Derulo Wakutana, Kifuatacho…..Bataaaarrrr

Jana tumeandika story ya Ay na Jason Derulo kuwa hatimaye watakutana kwa mara ya kwanza mjini Kigali, Rwanda.
Kwakuwa tumeshamla ngo’mbe mzima ni bora tuumalizie na mkia wake kabisa. Kuonesha picha yao wakiwa pamoja baada ya kukutana.
Kwanza wote wamefikia kwenye hoteli ya kifahari ya Serena. Wote wana jukumu zito la kuzikonga nyoyo za mashabiki wa nchini Rwanda watakaofurika kwenye uwanja wa Amohoro katika kilele cha mashindano ya muziki ya Primus Guma Guma Superstar.
Wamepata muda wa kupiga story za hapa na pale na bila shaka kuweka mipango ya kufanya collabo in the future, you never know! Isitoshe ilitokea tu Jason kumkubali AY hata kabla hajamwona na ndo maana aliahidi kumwangushia birthday party special. Hopefully, ahadi yake ataitimiza.
“Chillin with @jasonderulo in Serena Hotel- Kigali Rwanda#FAYAAA,” ametweet Ay alfajiri ya leo na kuambatanisha picha aliyopiga na msanii huyo wa ‘Whatchu Say’ na ‘What If.’
Jana pia AY alifanya interview na kituo cha radio cha KFM 98.7- Kigali Rwanda.
Meneja wake ambaye yupo nchini Ethiopia kwa sasa, Hemdee Kiwanuka, aliamua kuumuliza AY kama mambo yanaenda sawa kwenye trip yake hiyo ya Rwanda,”Are they treating you right without me there? Did you meet up with Joseph yet? He said he will come by & take you to the venue.”
“Everything is good bro,m enjoying,Ballin!!we spoke last night,m goin to meet with him later,” alijibu AY.
Now that’s what we call Starship. Ambwene yupo level zingine kabisa sasa hivi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents