Habari

Picha: Access Bank yazindua huduma ya bure ya utumaji fedha kwa njia ya simu ‘Rahisi’

Access Bank leo imezindua huduma iitwayo ‘Rahisi’ inayowawezesha wateja wake nchini kutuma fedha bure kutoka kwenye akaunti zao kwenda kwenye huduma za kifedha za simu zikiwemo M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Mwenyekiti Mtendaji wa Access Bank, Roland Coulon, akiwaeleza waandishi wa habari kuhusiana na huduma ya Rahisi
Mwenyekiti Mtendaji wa Access Bank, Roland Coulon, akiwaeleza waandishi wa habari kuhusiana na huduma ya Rahisi, kulia ni meneja masoko wa Access Bank, Muganyizi Bisheko

Pia wateja wa benki hiyo wataweza kutumia huduma hiyo kulipia huduma mbalimbali ikiwemo kulipia maji, ving’amuzi na umeme.

Mwenyekiti Mtendaji wa Access Bank, Roland Coulon, akikata utepe kuzindua huduma hiyo
Mwenyekiti Mtendaji wa Access Bank, Roland Coulon, akikata utepe kuzindua huduma hiyo

Akiongea na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika kwenye makao makuu ya Access Bank yaliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mtendaji wa Access Bank, Roland Coulon, alisema lengo la kuanzisha ‘Rahisi’ ni kuwezesha huduma za kibenki kuwa katika kiwango cha juu na zenye kupatikana kwa watu wote.

“Kwa Rahisi tunapanga kutengeneza viwango vipya katika kufikia huduma za kibenki kwa urahisi kabisa ukitumia simu yako ya mkononi na bure kabisa ukijiunga nasi,” alisema Coulon. “Hii ni huduma ya kwanza na ya bure ya utumaji fedha kwa njia ya simu nchini Tanzania.”

Mkuu wa Huduma za  Benki zisizo na matawi na Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo, Andrea Ottina (katikati) akifafanua jambo
Mkuu wa Huduma za Benki zisizo na matawi na Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo, Andrea Ottina (katikati) akifafanua jambo

Kwa upande wake Mkuu wa Huduma za Benki zisizo na matawi na Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo, Andrea Ottina alisema huduma ya Rahisi ni mapinduzi makubwa kwenye masuala ya kibenki nchini.

Ottina alisema mapinduzi hayo yamewezeshwa na uwezo wao wa kutengeneza mifumo yao wenyewe ya kompyuta ya ndani kwa ndani pamoja na ushirikiano na kampuni ya Selcom.

Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Tanzania, Sameer Hirji (katikati) akielezea ushirikiano wao na Access Bank
Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Tanzania, Sameer Hirji (katikati) akielezea ushirikiano wao na Access Bank

“Ushirikiano wetu na Selcom, umetuwezesha kutengeneza huduma imara na ya kuaminika ya kibenki kwa njia ya simu inayowezesha kufanya miamala mingi,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Tanzania, Sameer Hirji alisema huduma ya Rahisi ina utofauti mkubwa kuliko huduma za aina hiyo kutoka benki zingine nchini kwakuwa haina makato yoyote.

Meneja Mauzo wa Access Bank, Tabuley Njavike akielezea namna Rahisi ilivyo huduma ya kwanza na ya bure kwa kutuma fedha kwa njia ya simu
Meneja Mauzo wa Access Bank, Tabuley Njavike (kushoto) akielezea namna Rahisi ilivyo huduma ya kwanza na ya bure kwa kutuma fedha kwa njia ya simu

Mmoja wa wateja wakubwa wa Access Bank, Fatma
Mmoja wa wateja wakubwa wa Access Bank, Bi. Fatma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents