Shinda na SIM Account

Picha: Alikiba anavyokula bata na Gavana Joho

Huu unaweza ukawa ni muda muafaka wa Alikiba kusherehekea mafanikio ya ngoma yake ya Seduce Me.

Msanii huyo ameonekana katika picha ya pamoja ambayo ameiweka katika mtandao wa Instagram wakiwa kwenye Helkopta na rafiki yake wa karibu ambaye pia ni Gavana wa mji wa Mombasa, Hassan Joho.

“My brother thank you for hosting me and my team in Mombasa. @joho_001 #KingKiba,” ameandika Alikiba kwenye picha hiyo.


Alikiba (katikati) akitumbuiza katika kampeni za Gavana Joho

Kiba pia alikuwa akimfanyia kampeni kiongozi huyo ya kugombea katika mji huo wa Mombasa kabla ya uchaguzi uliofanyika August 8 ya mwaka huu na Joho ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini Kenya kushinda katika uchaguzi huo kwa takribani asilimia 90.

Katika uhaguzi huo Joho aliwabwaga wagombea wengine akiwemo Awiti Bolo, Suleiman Shabahal na wengine.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW