Picha aliyopost Makonda yaleta neema kwa mlemavu huyu

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam @baba_keagan Ijumaa hii ambayo waumini wa dini ya kiislamu duniani kote wanasherekea Eid, alipost picha mtandaoni akifanya mazungumzo na mlemavu mmoja ambaye hakutambulika jina lake mara moja.

Picha hizo ilizalisha mijadala mingi, ila mmoja kati ya watu ambao mtandaoni anatumia jina la S Zakwani aliandika ujumbe wa kutaka kumsaidia mlemavu huyo baiskeli mpya.

“Mheshimiwa nijulishe huyu mtu yupo wapi nimsaidie baiskeli mpya” aliandika kijana huyo ambaye hakuweka wazi anapatikana wapi.

Bongo5TV itafuatia kuona namna gani kijana huyo anakabidhiwa baiskeli hiyo.

Written and edited by @yasiningitu 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW