Michezo

Picha: All he does is win: Mayweather amdunda ‘dogo’ Canelo (Details)

Kwa sauti ya Dj Khaled, ‘All he does is win’. Floyd Mayweather aka Money jana ameendeleza rekodi yake ya kutoshindwa kwa kumtandika dogo wa Mexico Saul Alvarez aka Canelo.

article-2420981-1BD46C88000005DC-841_634x441

Katika pambano hilo, Alvarez alipewa tuition ya bure na Mayweather na kuonekana mwanagenzi tu ulingoni na kuionja shubiri ya kushindwa kwa mara ya kwanza katika historia yake.

article-2420981-1BD4724A000005DC-390_634x371
Hilo lilikuwa pambano lililompa mkwanja mrefu zaidi Mayweather kwa kuingiza dola milioni 41.5.

Kwa kuajimini, Mayweather alimchanganya Canelo mapema tu, kwa kumtandika makonde na kuonekana kama mabondia wengine vibonde aliowahi kuwadunda.

article-2420981-1BD47AF2000005DC-950_634x404
Kwa ushindi wa jana Mayweather ameendelea kutopigwa katika mapambano yake yote 45 aliyowahi kupambana

Mayweather alipewa point 117-111 na 116-112 na majaji wawili huku mmoja akijifanya kipofu kwa kumpa 114-114.

“Hakuna shaka, ni mpiganaji mkali, mpiganaji mwenye akili sana,” alisema Alvarez. “Hakukuwa na suluhisho kwake.”

article-2420981-1BD4765A000005DC-307_634x393

Pambano lilipoisha, Mayweather hakushangilia, alienda kwenye kona na kuungalia umati ulioenda kushuhudia.

article-2420981-1BD47D5F000005DC-507_634x431
Alvarez aliionja shubiri ya kushindwa kwa mara ya kwanza katika historia yake

Alvarez alitazamiwa kuwa mpinzani mkubwa kwa Mayweather na alijitahidi kulifanikisha hilo lakini hakuweza. Kama wengine, alishindwa kulifumbua fumbo hilo gumu.

article-2420981-1BD48402000005DC-211_634x408
Refa Kenny Bayles akimuonya Alvarez

Kabla ya pambano hilo, Alvarez alisema alikuwa na mbinu za mchezo kusolve ujanja wa Mayweather katika kujihami na mikono yake miepesi. Alisema kama ingeshindikana, alikuwa na mbinu zingine angezitumia kushinda pambano hilo.

Lakini hakuna mbinu yoyote iliyowezekana baada ya kuingia ulingoni na alipata jibu la jinsi Mayweather alivyo mnyama.

Watu 16,746 waliingia MGM Grand kushuhudia pambano huku wengine wakiwa Wamexico waliotaka kumshudia kijana wao.

1

2
Mayweather akiingia ulingoni, nyuma ni Justin Bieber

3
Lil Wayne akirap wakati Mayweather akiingia ulingoni, pembeni ni Justin Bieber

Alvarez alitajidi mno kulazimisha pambano hilo lakini muda wote alipokuwa akijaribu aliishia kukutana na makonde usoni.

5

6

8

Mpaka raundi ya nne, dogo alianza kupanic na kurusha ngumi iliyomkasirisha Mayweather, ambaye alichukia zaidi baada ya Alvarez kukutaaa kugusanisha gloves kuendelea na pambano.

7

Pambano hilo lilikuwa la bure kwa TV nchini Mixeco na inakadiriwa kuwa watu milioni 70 waliliangalia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents